Pentekoste – Uumbaji Mpya    

Maelezo ya kikuhani kuhusu uumbaji ndani ya Kitabu cha Mwanzo 1 yanaanza na mazingira ya hali ya ukiwa.  Giza kuu lilitanda juu ya utupu. Hatimaye, Roho wa Mungu akapaa juu ya uso wa ukiwa na Mungu anatokeza utaratibu  na mpangilio juu ya ukiwa uliokithiri. Mungu anatamka maana  katika uwepo; utaratibu wenye mpangilio huchukua nafsi ya utupu na ukiwa. Huu ndiyo mwanzo wa uumbaji ambao tunakumbuka uzao wake mara kwa mara wakati wa sherehe za mavuno na tafrija zingine tunaposherekea uumbaji. 

Kila mwaka, aidha tunakumbuka tendo la Mungu wakati wa mapambazuko ya uumbaji mpya. Watu waliokuwa na hofu wakiwa wamekusanyika kwenye Chumba cha Juu walihisi ujio wa nguvu za Roho Mtakatifu kuzindua uumbaji mpya. Roho anapaa juu ya machafuko mengine na kuleta hali ya utaratibu mpya ndani ya uumbaji. Kwa kupitia Mtume Petro, Mungu anatangaza Habari Njema ya wokovu uliowezekana kwa Bwana mfufuka na kanisa likajielewa kwa undani zaidi. Ama,  kama tunavyopenda kusema, ukawa mwanzo wa uwepo wa kanisa. Kile kilichokuwa ndani ya mawazo ya Mungu tangu kabla ya uumbaji unajidhihirisha wazi mbele ya ujio mpya mwenye nguvu ya Roho Mtakatifu. 

Hii ndiyo sababu tunasherekea wakati wa Pasaka. Mungu haachilii ulimwengu wenye machafuko. Kutokana na upendo wake wa dhati haiwezi ikatokea yeye kuachilia ulimwengu.  Mungu hufanya upya ulimwengu na kufungua mlango wazi kwa maisha mapya kwa wale wote watakakaojuliza, “Tufanye nini basi?” Kusikia jibu la Mungu, mioyo yetu huangazwa na kupata hekima ya kusema, ” Sasa tunageuka, sasa tunatubu.” Baada ya hapo tunajibwaga ndani ya maji matulivu ili kujumuishwa ndani ya Kristo. 

Kwa kubatizwa na Mungu wa utatu, tunapata nguvu za kimiujuza za yule anayefanya ya kale kuwa mapya. Mungu huweka umilele ndani ya mioyo yetu. Tunagundua sio tu kufanywa upya utambulisho wetu binafsi. Bali pia tunapambanua kina na upana wa mahusiano tulio nayo. Sisi tu zaidi ya mtu binafsi; tu watu kwa ujumla. Tukiwa pamoja na watu wengine, ndipo tunapata furaha ya kushiriki katika jamii mpya. Tunapo batizwa ndani ya maji, tunahisi kushuka kwa Roho yule yule aliyemshukia Yesu pale mtoni Yordani.  

Roho Mtakatifu hutuongoza katika kutubu dhambi na kumrudia Mungu ndani ya Kristo na kupata ule uumbaji mpya tuliyoahidiwa. Tunashiriki utu mpya inayotoka kwa Mungu. Jamii hii mpya inayoinukia imejikita ndani ya makusudi ya Mungu;  hiki ni chombo muhimu mkononi mwa  Mungu kuangazia nuru ulimwenguni kwa kutumia ujumbe wa Injili na kuujaza ulimwengu na  utukufu wake. 

Pentekoste kwa kweli ni wakati wa kusherekea. Kwa kusherekea kwetu, laiti watu wengine waliokuwa mbali na Mungu waje wapate furaha na mabadiliko yanayoletwa na Pentekoste. 

Neville Callam
Katibu Mkuu
Baptist World Alliance

(Translated into Swahili  by: Harrison Olan’g)