Mlipuko Unaobadilisha Maisha

Maporomoko ya Maji! Yanaweza kuwa ya ukubwa na umbo mbali mbali lakini mara nyingi huvutia macho. Ni maporomoko machache yakiwepo yanaweza kushinda yale ya Foz do Iguacu kule Parana, Brazil. Uhalisia wa wigo wa maporomoko! Mamilioni ya lita za maji yanayoporomoka juu ya jabali. .

Maji yanayotiririka mfululizo, kilometa baadaa ya kilometa, mwaka baada ya mwaka! Pamoja na uzuri ulo dhahiri na mchanganyiko wa mwonekano,unamkumbushia mtu nyakati maalum za historia ya wokovu.

Nyakati zingine, maporomoko ya maji yanaamsha hisia za mwanzo wa uumbaji wakati Mungu alipotenganisha maji ya ukiwa na kuumba dunia. Mungu aliumba anga kufanya viumbe vinawiri and na kusitawi, kila moja ikitunza nyingine ndani ya bustani ya uzima iliyositawi vizuri.  

Mara nyingine, maporomoko ya maji yanaamsha hisia za safari ya maisha kwa maji yanayotisha na kudhihirisha udhaifu wetu, lakini pia kufungua macho yetu kuona ukuu wa neema kwa watu ambao Mungu anawachagua. Wana wa Israeli walivuka juu ya maji yaliyochafuka bila madhara. Walipitia safari iliyotakatifu waliyosafiri watu wa Mungu katika historia yao yote chini ya ulinzi wa yule ambaye anaweza kutuokoa kutoka maangamizi na hatari.

Hasa mwisho wa safari, katika njia iliyochongwa na mapitio ya wanadamu yenye urefu upatao kilometa mbili pembezoni mwa mlima unao akisi uzuri huo usiku na mchana, maporomoko ya maji huacha kutiririka. Maporomoko hayo huonekana kwa mbali kwa muonekano unaofanana na miamba na hatimaye kudondoka ardhini. Maporomoko hudondoka kwa umbali na kwa kasi inayorusha maji yanayomrukia kila anayethubutu kusogea karibu nayo.

Maporomoko hayo yanaweza kumkumbusha mtu mlipuko unaotokea ndani ya mimba kwa wale Mungu anaowajalia kuzaa watoto. Maji hulipuka na kutokeza maisha mapya pamoja na usiri, ahadi na matumaini.

Kwa habari za Mariamu, akiwa bado kijana mdogo, alikumbana uso kwa uso na siri wakati yule mjumbe mtakatifu alipomwambia kitu kizuri, lakini chenye kutisha, kitu ambacho Mungu alikuwa akifanya ndani yake. Maneno ya kushutua yalitokeza muitikio tulivu wa utayari kufuata mapenzi ya Bwana.

Baadaye, pale Bethlehemu, ndani ya hiyo siku kubwa ya kukumbuka, maji yalilipuka na kukatokea kiumbe cha miujiza aliyemlaza katika hori la kulia ng’ombe. Yeye aliyezaliwa katika uharibifu, kuonekana kwake kulisababisha mlipuko mkubwa katika historia ya wanadamu.

Akilia kama vile watoto wachanga waliavyo Yesu aliachana na usalama aliyokuwa nayo ndani ya tumbo la mama yake mpendwa na kukabiliana na ulimwengu uliojaa maovu. Alianza kwa kujifunza uchungu wa maisha kama mkimbizi. Baadaye alitangatanga kama mtu asiye na makazi maalum. Aidha, hatimaye alitoa uhai wake kama fidia ya haki. Wakati huo huo alionyesha jinsi upendo unavyotawala maisha, jinsi msamaha unavyofunika dhambi, na jinsi uzima wa milele unavyoshinda tishio la kifo.

Maji yale yaliyochuruzika jioni ya Krismasi ya kwanza yalifungua njia ya uzima ambayo hata kifo haiweze kuharibu. Hata Kalvari haikuweza kuondoa ule uzima; na ikabaki tu njia ya kufikia kaburi tupu. Kifo kikapisha ushindi wa ya ufufuo.

Tuseme nini basi, zaidi ya hayo yote, maporomoko ya Iguaçu yanakumbusha habari njema kwamba Krismasi ni mlipuko ndani ya wakati na mahali, mlipuko mkubwa kupitia maji yabubujikayo kutoka kwenya mimba ya mama aliye bikira. Maporomoko hayo yanahusu mabadiliko makubuwa katika historia, tukio la kihistoria ambayo ina nguvu ya kubadilisha muelekeo wa maisha ya kila mtu na jamii kwa ujumla.

Mtoto tunayesherekea kuja kwake ni Emanuel, Mungu yu pamoja nasi! Je habari hii tukufu ya Krismasi imebadilishaje maisha yako na ya wale uwapendao?

Neville Callam
Katibu Mkuu
Ushirikiano wa Dunia ya Wabatisti

(Translated by/Imetafsiriwa na : Harrison G. Olan’g)